Tanzanian star Shilole has opened up on going through domestic abuse at the hands of her husband Ashrafu Sadiki alias Uchebe.

Taking to her social media platform, Shilole apologized to the family and other domestic abuse victims for not having opened up early.

'Naandika haya, nikiwa na akili timamu na utulivu, La kwanza kabisa nataka KUOMBA RADHI JAMII YANGU.

Naomba radhi kwa sababu niliwaaminisha ndoa yangu haina tatizo, huku ukweli ukiwa hauko hivyo, nimekuwa mtu wa kuambulia vipigo na MENGINE yasiyozungumzika, Naomba radhi kwa sababu niliposikia wanawake wenzangu wakipigwa niliwaambia PAZENI SAUTI.

Niliposikia mwanamke kule Kigamboni ameuwawa na kuchomwa moto niliomboleza na jamii na kusema Bora angesema".. huku mimi nikijikausha na kujitoa kwenye kundi lao wakati ukweli wangu MIMI NI MWENZAO, Naomba radhi. '

Shilole added that one of the reasons she decided to speak up is because she is a mirror in the society.

'Mimi ni kioo cha jamii, tena sura kubwa ya wanawake.

Leo numeona nivunje ukimya kwa kuweka wazi kwamba MUME WANGU ASHRAFU SADIKI, maarufu kama UCHEBE AMEKUWA ANANIPIGA SAAANA, na tena hata baada ya kunipiga hajali kupiga simu wala kujua naendeleaje, nauguzwa na watu baki hospitali, na bado manyanyaso mengine yanayoikosesha hii ninayoiita Ndoa uhai na furaha

na zaidi nina WATOTO, watoto wanaoniangalia kama Baba na Mama, leo nikubali kufa na kuacha wanangu barabarani, SITAWEZA .

She added that she had persevered so much with her husband but added she was tired.

'Uchebe' ni mwanaume niliyempenda, nilimvumilia kwa madhaifu yote, nikampa kila kitu, (Utu wangu, Mali Zangu.

Na hata palipotakiwa kumuendeleza asimame mwenyewe nilifanya kwa kuwa nilidhani tuko pamoja.

lakini HILO HALIKUWAHI KUZUIA VIPIGO, DHARAU NA USALITI.

Siku 2 zilizopita baada ya kutoka SABASABA KUTAFUTIA WATOTO WANGU NA KUMTAFUTIA YEYE NILIPIGWA SANA.

SABABU ZA KUPIGWA NI MIGOGORO MIDOGO YA KAWAIDA AMBAYO IPO KWENYE KILA NDOA, sio kwamba amenifumania au mambo yanayoshindwa kuzungumzika, hapana, Tena Namuheshimu sana, lakini solution aliyoiona ni kunipiga kinyama bila huruma.

Tena kwa kunishtua na ngumi nikiwa usingizini, Kama mnavyoona picha hapo ni matukio ya siku tofauti tofauti.

She added,

'Najua nitalaumiwa kwa kuweka hill mtandaoni, ILA SINA NAMNA, MAISHA YANGU NI MAISHA YA WATU KWA KIASI KIKUBWA, JAMII INANITAZAMA KAMA MFANO..

Nimefika mwisho, na kuanzia sasa naomba nisitambulike kama Mke wa Uchebe, ila Mama aliyeamua kuweka maslahi ya watoto wake mbele na kuamua kuwa mwenyewe kwa usalama na furaha yake

Wakati nahangaikia mambo yangu ya ndoa, post hii itumike kuwakumbusha wanawake TUVUNJE UKIMYA, TUPINGE UKATILI, TUTAKUJA KUULIWA.

Like Shilole advises if going through abuse, please speak up.