Stevens Muendo, editor with Standard Group, Kenya. Creative writer key on Entertainment, Travel, Adventure, Investigative and Human Interest issues. (According to his twitter profile) is on the receiving end of Coast based blogger who has called him out for writing false stories and not giving coast region entertainment scene a priority, but instead write about D-list celebrities who are not known by anyone in return of monetary and sexual favors.

Speaking to Steve this afternoon, he said;

Coast artists will always complain, no one gives them coverage like pulse does.

10530842_10152304958726723_6241520635965128927_n

Anyway below is the post  written in Swahili by the Coast blogger.

Inashangaza na kusikitisha sana jinsi wahariri wenu wa habari wanavyoangazia habari za kutoka hapa mkoani pwani. Acha nianze na tamasha kubwa kwa jina Stylus DJ Awards iliyofanyika katika hoteli ya kifahari ya Whitesands. Tamasha hio kama desturi Steve Muendo alipotezea. Iliyofata ni tamasha ya Celebrity Affair ambayo Ilifanyika katika ukumbi wa Skylux Sports Pub kule Mtwapa na hata wakati Tamasha hio ikifanyika mhariri wenu kwa jina Steve Mwendo alikuepo hapa mkoani pwani siku hio lakini alijifanya kutokua na habari. Tamasha ya tatu ni ya Miss Pwani Gala ambayo ilifanyika wiki jana katika ukumbi wa Sheba Lounge pale city mall lakini hio pia vile vile pulse mlijitia kutokua na habari..
Sasa cha kushangaza ni kua wahariri wa pulse magazine hujitia hamnazo tamasha kubwa kama hizi zinapofanyika hapa mkoani pwani. Yashangaza sana kuona jarida lenu laruhusu kuweka habari kua model na msanii chipukizi kwa jina Sandra ambae hana nyimbo hata moja ameandalia mamake birthday party. Ukitizama katika ukurasa wake wa Fcbk utaona jinsi rafiki zake wanavyoshangaa baada ya pulse kusema ni muimbaji manake hana nyimbo hata moja na anachoweza kuimba ni (happy birthday to you) pekee kulingana na jamaa wake Hassan Faisal. Kwani hua mfanyi uchunguzi mwanzo kabla muangazie jambo ama Pulse sasa ni ya marafiki na wapenzi wa waandishi wenu? Mhariri wenu mrongo kwa jina Mkala Mwaghesha aliweza kudanganya jinsi sherehe hio ilivyo hudhuriwa na wasanii wote bila ya kutaja hata mmoja kwa jina wala hata kutuwekea picha ya kuthibitisha madai hayo isipokua kutuwekea picha ya vibofu. Ukisoma habari hio utaona alivyoeleza mipango alionayo chipukizi huyo asiyejulikana kabisa. Habari hizo za birthday mrembo huyo ilifaa ajiandikie kwa kurasa lake la Facebook au twitter kwa jamaa na rafiki zake na wala sio kuangaziwa kwa Pulse manake hazihusiani kabisa na burudani ya hapa mkoani.
Mbona muangazie mipango ya chipukizi asiyejulikana ilihali wanaofanya mambo ya kikweli yanayo onekana hamuangazii?
Sasa swali ni je wahariri hawa wenu hua Lazima wahongwe mwanzo ndipo waweze kuandika habari ama mrembo huyo amewapa uroda ndio maana anaangaziwa kila wakati? Yaani dunia nzima ikitaka kupata habari za burudani kutoka hapa mkoani kupitia jarida lenu mwapeana habari za birthday ya Mamake underground halafu huyu mwanada hii ni Mara ya tatu Pulse yamuangazia msichana huyu wa majivuno ambae alitukana wasanii na hakuna lolote amefanya, acheni kutuzengua. Peace am OUT.

10313515_10205155687918955_368797692731859583_n
The article that was done by Pulse’ writer Mkala Mwangesha
MPASHO TV