MKE YUWANINYOROSHA: The Late Ahmed Darwesh's Brother Makes Explosive Admissions Online

Piece by: Grace Kerongo
Lifestyle

The late brother is breathing fire. Khamis Darwesh, also a journalist has come out to add more fuel to the already fanned flames razing across the nation, this is after the recent back and forth between President Uhuru Kenyatta and Governor Hassan Joho.

Khamisi penned a shairi that spews subtexts and chini ya maji jabs towards the whole incident that saw Uhuru tell Joho.

"I'm not your wife, so stop following me around!"

This was after the head of state ordered the Coast kingpin and ODM deputy chief placed under office arrest. Joho was blocked from attending Uhuru's ceremonial reopening of the Likoni Ferry crossing and relaunch of MV Likoni.

Khamisi being a Joho diehard, took to social media to write a poem about a "wife".

Read it below...

MKE YUWANINYOROSHA

Tangu kukwambia kweli, kuwa mambo waharibu,

Mke wangu hunijali, washinda kuniadhibu,

Leo unazuwa hili, kesho lile wajaribu,

Mke wangu taratibu, punguza kuninyorosha.

Mke umemea pembe, mkali sana ajabu,

Na hao wako wapambe, hawana ustarabu,

Wanakugawia wembe, unichane ja kitabu,

Mke wangu taratibu, punguza kuninyorosha.

Dhuluma unazofanya, unataka niwe bubu,

Katu nisije kukanya, nimezee masaibu,

Hata unaponifinya, ninyamaze bubububu,

Mke wangu taratibu, punguza kuninyorosha.

Kwa ubaya wanisema, jina langu kuharibu,

Eti miye sijasoma, naona wajipa tabu,

Biashara waninyima, kote waeka bawabu,

Mke wangu taratibu, punguza kuninyorosha.

Mimi si nyama ni mtu, kuwache kuniadhibu,

Kuwatetea wa kwetu, ndio'we unisulubu?

Uwapige na viatu, nikwangalie swahibu!,

Mke wangu taratibu, punguza kuninyorosha.

Wapendelea wa kwenu, wale nyama na kababu,

Wapika bonge la menu, kwa wako ndugu na babu,

Mezijua njama zenu, wa kwangu wapate tabu,

Mke wangu taratibu, punguza kuninyorosha.

Ukweli umekuchoma, usingejawa ghadhabu,

Naapa sirudi nyuma, hilo amini muhibu,

Kwa zako mbovu kalima, wanijenga huharibu,

Mke wangu taratibu, punguza kuninyorosha.

Ndimi wako Sultani, haya niliyekutubu,

Wala sinayo huzuni, kwa hizi zako dharubu,

Itakwisha mitihani, kwa uwezo wa Wahabu,

Mke wangu taratibu, punguza kuninyorosha.