Journalist Mohamed Ali has never been one to mince his words and he often says what he damn well pleases. I guess that is why his investigative piece ‘Jicho Pevu’ was always such a hit. Whatever the case may be, he took issue with all the religious leaders invited to the Jubilee government’s celebration at Afraha Stadium, Nakuru.

Unless you live under a rock, you probably know that the six Kenyans who had cases at the  ICC, had all charges against them dropped due to lack of evidence or a plethora of other such reasons. The thanksgiving rally has elicited mixed reactions, but President Uhuru Kenyatta and his Deputy William Ruto were not too shy to celebrate the fact of the matter at Afraha Stadium in Nakuru.

This is what Mohammed Ali had to say about the entire affair:

 Kesho wanahabari kahawa watapachika kamera zao kila kona kupeperusha matangazo hayo ya moja kwa moja kutoka uwanja huo. Nawaita wanahabari kahawa kwasababu chai walioinywa katika ikulu ya Nairobi iligeuza fikra na taaluma na kuwafanya wanahabari wa kutangaza sifa, mavazi na makalio ya wanawake. Siku itakayofuatia baada ya sherehe hizo, magazeti za humu nchini zitatwaa picha za wawili hao na kuwafananisha na mashujaa licha ya wao kujua wazi kuwa huo utaonekana kama kejeli kwa wakenya na familia za waathiriwa wote wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007. Kesho wanahabari watawasahau kina mama waliobakwa, kina mama na watoto walioteketezwa ndani ya kanisa la Kiambaa, familia moja iliyopigwa moto ndani ya nyumba yao huko Naivasha.”

 

He went on to accuse religious leaders, who attended the thanksgiving service, of being blinded by their love for money.

 

“Viongozi mbali mbali wa dini senti watafika katika uwanja huo sio kumsifu Mungu bali kusifu senti zisizo na adabu. Nawaita viongozi wa dini za senti kwa sababu nina machungu na tabia ya viongozi hawa. Wamekuwa ni watu wa kuhubiri meno badala ya neno. Leo nina machungu maana kwa ufupi tunaambiwa kuwa zaidi ya wakenya elfu moja waliouawa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi walijiuua wenyewe kwa hiari yao. Walitaka kubakwa wenyewe kwa hiari yao, walitaka kufumwa mishale kwa hiari yao, walitaka kuchomwa kwa hiari yao, walitaka kukatakatwa kwa mapanga kwa hiari yao

Je, mnaokwenda kuhudhuria mkutano huo na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu hamuogopi? Hamuogopi Mungu japo kwa sekunde? Mmewasahau waliouawa haraka hivi? Nauliza kwa upole na unyenyekevu bila ya chuki kwa mtu yeyote. Endeleeni maana Kenya mungu wake ni ukabila, endeleeni lakini mkae mkijua Mungu ndiye Mkuu na kwake haki itapatikana. Sisemi ni makosa kuhudhuria sherehe hizo. La hasha! Ninachosema ni kuwa hatuwezi sherehekea uhuru wa watu wawili dhidi ya haki ya watu zaidi ya elfu moja.”

MPASHO TV